MSHUKIWA WA WIZI WA MIFUGO KUFIKISHWA MAHAKAMANI KAPENGURIA.


Mshukiwa mmoja wa wizi wa mifugo anatarajiwa kufikishwa leo katika mahakama ya kapenguria kaunti hii ya pokot magharibi kujibu mashitaka ya kupatikana na mifugo wanaoshukiwa kuwa wa wizi katika gari lake eneo la marich.
Kamanda wa polisi Pokot ya kati Bamford Surwa amesema kuwa polisi walishuku mienendo ya jamaa huyo baada yake kudinda kusimamisha gari aina ya Probox katika kizuizi cha polisi ili kukaguliwa kabla ya kuendelea na safari yake hali iliyolazimu polisi kufyatulia risasi magurudumu ya gari hilo kabla ya kupatikana na kondoo na mbuzi wanaoshukiwa kuwa wa wizi.
Surwa amesema mshukiwa atafikishwa mahakamani kushitakiwa kwa makosa ya kumiliki mali inayoshukiwa kuwa ya wizi kutokana na hali kuwa amedinda kueleza iwapo ndiye mmiliki halisi wa mifugo hao au la na kwa nini alidinda kusimama alipotakiwa kufanya hivyo.
Surwa ametoa wito kwa wananchi kutokuwa na mazoea ya kukaidi maagizo ya maafisa wa polisi bali kushirikiana nao kila wanapotakiwa kufanya hivyo ili kurahisha majukumu yao ya kuhakikisha usalama wa mwananchi.