MSHIRIKISHI WA UTAWALA ENEO LA BONDE LA UFA GEORGE NATEMBEYA AJIULUZU

Mshirikishi wa utawala eneo la bonde la ufa George Natembeya hatimaye ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ili kuzingatia safari yake ya kugombea ugavana wa kaunti ya Trans nzoia katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu.
Natembeya ambaye ni afisa wa umma wa kwanza kutangaza kujiuzulu, ameondoka rasmi baada ya kuhudumu katika wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 25.
Katika hotuba yake ya kujiuzulu mshirikishi huyo wa bonde la ufa ameelezea ufanisi wake katika kuhakikisha visa vya mimba za mapema vinapungua eneo hilo, kukabili utovu wa usalama mipakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti ya Turkana miongoni mwa maswala mengine.
Juma lililopita Natembeya alitangaza kuwa angejiuzulu mapema ili kutoa nafasi kwa mshirikishi atakayeteuliwa kuchukua nafasi yake kujiandaa mapema katika kuhakikisha usalama unadumishwa eneo hilo mbele ya uchaguzi mkuu ujao.