MRADI WA USAMBAZAJI WA MAJI WAZINDULIWA NAMUTOKHOLO KAUNTI YA BUNGOMA.


Wakazi wa eneo la Namutokholo eneo bunge la Sirisia kaunti ya Bungoma wamepata afueni baada ya serikali ya kaunti kuzindua mradi wa usambazaji maji eneo hilo mbalo limeshuhudia uhaba wa maji kwa kipindi kirefu.
Akizindua mradi huo waziri wa huduma za umma katika kaunti ya Bungoma Sabwami Keya amesema kuwa utawanufaisha wakazi hata zaidi.
Afisa mkuu katikia idara ya maji Rosalia Soita amesema kuwa maji hayo yatasambazwa kwenye maeneo mbali mbali ambayo yanakabiliwa na uhaba wa bidhaa hiyo muhimu.
Wakazi wa eneo hilo wameusifia pakubwa mradi huo ambao wamesema utawapunguzia zaidi kina mama mwendo mrefu wa kutafuta maji.