MRADI WA UCHIMBAJI VISIMA WAZINDULIWA POKOT MAGHARIBI

Gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo amezindua rasmi mradi wa uchimbaji visima maeneo mbali mbali ya kaunti hii katika shughuli iliyofanyika eneo la Riwo.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Lonyangapuo amesema kuwa mradi huu umechelewa kwa miaka miwili baada ya mitambo ambayo inatumika kuchimba visima hivyo kuharibika, kando na mvua kubwa iliyoshuhudiwa mwaka jana na kupelekea maporomoko ya ardhi.
Aidha Lonyangapuo amesema kuwa serikali yake imeweka mikakati ya kununua mtambo mwingine ambao utatumika kuchimba visima baadaye mwaka huu ili kurahisisha shughuli hiyo.