MRADI WA KENYA CLIMATE SMART WAINGIA AWAMU YA NNE POKOT MAGHARIBI.


Mradi wa kilimo wa Kenya climate smart agriculture project ambao unaendelezwa katika kaunti hii ya Pokot magharibi kwa nia ya kuwawezesha zaidi wakulima, umeanza awamu yake ya nne ya kutoa mifugo kwa makundi mbali mbali ya wakulima kaunti hii.
Mshirikishi wa mradi huo katika kaunti hii Philip Ting’aa amesema kuwa katika awamu hii ya nne tayari wamefikia makundi 175 makundi 600 yakilengwa huku mbuzi alfu 1,555 wakitarajiwa kutolewa kwa makundi hayo pamoja na kondoo zaidi ya alfu moja akisisitiza umuhimu wa kununuliwa mbuzi wa kiume.
Kando na kutoa mifugo kwa ajili ya makundi hayo ya wakulima, Ting’aa amesema kuwa mradi huo pia unaendeleza mpango wa unyunyiziaji maji mashamba katika maeneo mbali mbali ya kaunti hii ya Pokot magharibi ikiwemo ule wa chepkotii, kigen na chepsebin.
Ametoa wito kwa wakulima kukumbatia kikamilifu miradi hiyo kwani itawasaidia kuimarisha uzalishaji na kuongeza mapato yao hali itakayokabili umasikini miongoni mwa wakulima kaunti hii.