MPASUKO WA ARDHI UMESHUHUDIWA KATIKA ENEO LA CHESEGON KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI


Wakaazi wa eneo la Chesegon eneo bunge la Sigor kaunti ya Pokot Magharibi wanaishi kwa hofu baada ya kushuhudiwa mpasuko ardhini kukiwa na uwezekano wa mporomoko wa ardhi.
Kwa mujibu wa Tito Lopuriang mmoja wa wakaazi hao ni kuwa tukio hilo linawapa wasiwasi ikizingatiwa kwamba eneo hilo lilikumbwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi mapema mwaka huu hivyo hatua za tahadhari zinapaswa kuchukuliwa mapema.
Kufuatia hayo serikali ya kaunti ya Pokot Magharibi na ile ya kitaifa zimetakiwa kuwatuma wataalam katika eneo hilo kutathmini hali na wakaazi kuhamishiwa sehemu salama kabla ya kutokea mkasa.