MPANGO WA UJI KWA SHULE ZA CHEKECHEA WAKOSOLEWA NA VIONGOZI POKOT MAGHARIBI.

Na Benson Aswani
Siku moja baada ya gavana wa kaunti hii ya Pokot magharibi John Lonyangapuo kuzindua mpango wa kuwapa uji wanafunzi wa shule za chekechea, baadhi ya viongozi katika kaunti hii wamekosoa pakubwa mpango huo.
Wakiongozwa na mwakilishi wadi maalum Elijah Kasheusheu, viongozi hao wamedai kuwa gavana Lonyangapuo anatoa kipau mbele kwa maswala yasiyo na umuhimu mkubwa hali yapo maswala mengi ambayo yanahitaji kushughulikiwa kwa dharura ikiwemo uhaba wa dawa katika hospitali za kaunti hii pamoja na upungufu wa madaktari.
Aidha Kasheusheu amedai kuwa gavana lonyangapuo anatumia mradi huo kupora fedha ambazo atatumia katika kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.