MPANGO WA KUTOA CHAKULA SHULENI ENEO BUNGE LA KACHELIBA WAENDELEZWA.


Serikali inaendeleza mpango wa kutoa chakula kwa shule za msingi katika kaunti hii ya Pokot magharibi katika juhudi za kuhakikisha kuwa wanafunzi wanahudhuria masomo bila tatizo lolote.
Hii ni baada ya kubainika awali kuwa jamii nyingi za kaunti hii zinakumbwa na changamoto ya kupata chakula hali ambayo inawafanya wanafunzi wengi hasa katika shule za msingi kukosa fursa ya kuhudhuria masomo shuleni.
Mkurugenzi wa elimu eneo la Kacheliba Edward Wangamati amesema kuwa kwa sasa wanaendeleza mpango wa kusambaza chakula katika shule za msingi eneo hilo akisisitiza kuwa kila shule itapokea chakula kulinganma na idadi ya wanafunzi.
Kuhusu swala la mtaala wa umilisi CBC, Wangamati amesema kuwa mikakati imeendelea kuwekwa kuhakikisha kuwa mtaala huo unafanikishwa ikiwemo ujenzi wa madarasa zaidi katika shule mbali mbali akiwataka wazazi kuukumbatia kwanu una manufaa makubwa.