MPANGO WA KUJENGWA KAMBI YA KDF ENEO LA TIATI WAENDELEA KUIBUA HISIA.

Viongozi eneo bunge la Tiati kaunti ya Baringo wanazidi kutoa kauli zao kuhusu pendekezo la serikali la kutaka kutengwa kipande cha ardhi eneo bunge hilo ili kuwezesha mpango wa kujengwa kambi ya utoaji wa mafunzo kwa makurutu wanaojiunga na kikosi cha ulinzi KDF.

Mwakilishi wadi ya Tangulbei Shadrack Mailuk amewataka wakazi kutokuwa na wasiwasi akisema kuwa pendekezo hilo haliwezi kutekelezwa hadi wenyeji watakapohusishwa na kukubaliana na mpango huo.

Mailuk amewataka wenyeji kupuuza taarifa zinazoenezwa kwamba kuna ardhi ambayo tayari imetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kambi hiyo akisema kwamba bado mazungumzo yanaendelea.

Hata hivyo mwakilishi wadi ya Tirioko Sam lokales amesema kama viongozi kutoka eneo bunge hilo hawatakubali ardhi ya wakazi kutwaliwa huku akitishia kuwasilisha kesi mahakamani kupinga mpango huo.