MOROTO APONGEZWA KWA UJENZI WA BARABARA ENEO BUNGE LA KAPENGURIA


Mwenyekiti wa mamlaka ya barabara za maeneo ya mashinani KERA eneo bunge la Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Andrew Kodokwang amepongeza kujengwa barabara ya kutoka Limang’ole kupitia Cheptarama hadi shule ya msingi ya Kiruru.
Kodokwang amesema kuwa haingetabirika kuwa barabara inaweza jengwa eneo hilo la mlima, akimpongeza mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto kwa juhudi zake ambazo zimepelekea kujengwa barabara hiyo.
Aidha Kodokwang amesema kuwa nafasi ya Moroto katika kamati ya bunge la taifa kuhusu bajeti na matumizi imewezesha kujengwa barabara kadhaa eneo bunge la kapenguria.