MOROTO APINGA KUFUNGWA ZAHANATI MAENEO YA MASHINANI


Mbunge wa Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto amekosoa hatua ya kufungwa baadhi ya vituo vya afya kaunti hii hasa maeneo ya mashinani.
Akizungumza na kituo hiki Moroto amesema kuwa huu si wakati wa kufungwa vituo vya afya hasa kutokana na ongezekeo la maambukizi ya virusi vya corona nchini, akisema huenda hatua hii ikawa pigo kwa vita dhidi ya janga hili.
Aidha Moroto amemtaka waziri wa afya kaunti hii na kamati ya bunge la kaunti kuhusu afya pamoja na usimamizi wa afisi ya gavana kufanya uchunguzi mashinani kuhusu swala hilo kabla ya hatua zozote kuchukuliwa.