MOROTO APATA AFUENI BAADA YA KUTUPILIWA MBALI KESI INAYOHUSU SHAMBA LA ADC.


Mbunge wa Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi Samwel Moroto amepata afueni baada ya kukamilika kesi iliyokuwa ikimwandama katika mahakama ya Kitale iliyokuwa ikihusu shamba la ustawishaji wa kilimo ADC.
Akizungumza baada ya uamuzi wa kumwondolea mashitaka hayo, Moroto ameipongeza mahakama kwa uamuzi huo ambao amesema kuwa umezingatia haki akisisitiza hakutekeleza makosa anayotuhumiwa nayo na kuwa shutuma dhidi yake zilichochewa kisiasa.
Wakati uo huo Moroto amepongeza pande husika katika kesi hiyo kwa ushirikiano ambao ulipelekea kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Ni uamuzi ambao umepongezwa na baadhi ya viongozi pamoja na wakazi wakiongozwa na kiongozi wa vijana kaunti hii ya Pokot magharibi Richard Todosia pamoja na mwakilishi maalum Elijah kasheusheu almaarufu ozil ambao wamesema haki imefanyika.