MOROTO AKOSOA OPARESHENI DHIDI YA MICHEZO YA KAMARI.


Mbunge wa kapenguria kaunti ya Pokot magharibi Samwel Moroto amekosoa oparesheni inayoendeshwa na idara ya usalama katika kaunti hii dhidi ya michezo ya kamari.
Akizungumza na kituo hiki Moroto amesema kuwa wamiliki wa vyumba vya kucheza michezo hiyo wamewekeza pakubwa katika michezo hiyo na iwapo itasimamishwa itaathiri pakubwa mapato ya wakazi wengi kaunti hii.
Badala yake Moroto amependekeza kubuniwa sheria za kudhibiti michezo hiyo ili kuhakikisha inaendeshwa kisheria na kuwaruhusu wakazi wanaojipatia kipato cha kila siku kuendeleza biashara hizo kwa njia ya halali.
Wakati uo huo Moroto ameshutumu utekelezwaji wa oparesheni hiyo anayodai kuwa ni kinyume cha sheria kutokana na hali kuwa wakazi hawajahusishwa kabla ya kuanza kuitekeleza.