MOROTO ADAI POLISI WANATUMIKA KUWAHANGAISHA WAKAZI KATIKA ARDHI YA CHEPCHOINA.


Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ameendelea kukashifu kila amedai maafisa wa polisi kutumika kuwahangaisha wakazi kwenye ardhi yenye utata ya Chepchoina mpakani pa kaunti hii ya Pokot magharibi na kaunti jirani ya Trans nzoia.
Moroto amedai kuwa maafisa wa polisi wamekuwa wakitumika kuwafurusha wakazi kwenye ardhi hiyo na mabwenyenye ambao lengo lao ni kuinyakua husika.
Wakati uo huo Moroto amewataka wakazi kwenye ardhi hiyo kuendelea kusalia pamoja na kushirikiana huku akiahidi kuzidishwa juhudi za kuhakikisha kuwa suluhu inapatikana kutokana na tatizo hilo ambalo limekuwepo kwa muda sasa.
Aidha Moroto amesisitiza haja ya kuwepo mazungumzo ya kutafuta sluhu kutoka pande zote mbili kaunti hii na kaunti ya Trans nzoia ili kutafuta suluhu ka masaibu yanawakumba wakazi wa eneo hilo jinisi ilivtyofanywa maeneo mengine kanda hii.