MKUTANO WA AMANI BARINGO WAENDELEA KUIBUA HISIA MIONGONI MWA VIONGOZI


Hisia mbali mbali zimeendelea kuibuliwa na viongozi kanda ya kaskazini mwa bonde la ufa kufuatia orodha iliyotolewa ya wamiliki wa silaha haramu kanda hii katika mkutano wa amani uliofanyika eneo la Chemolingot kaunti ya Baringo siku ya jumamosi.
Mwakilishi wadi ya Tirioko kaunti ya Baringo Sam Lokales ameelezea kuunga mkono orodha hiyo akisema ni ya kweli huku akitoa wito kwa wote waliotajwa katika listi hiyo kujitokeza na kusalimisha bunduki hizo katika kipindi hiki ambacho kimetolewa na serikali.
Aidha Lokales amesema wanalenga kuwatumia wakazi wa maeneo ambako waliotajwa katika orodha hiyo wanatoka ili kuhakikisha kuwa wahusika wanapatikana na kusalimisha bunduki hizo katika juhudi za kuafikia usalama maeneo haya.