‘MKONO WA MUNGU NDIO UTAMWOKOA MUKENYANG’ ASEMA ARAULE


Itahitaji muujiza kwa spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi Catherine Mukenyang kuokoka kutokana na hoja ya kubanduliwa afisini inayotarajiwa kujadiliwa hii leo na bunge la kaunti hii.
Haya ni kulingana na mwakilishi wadi ya mnagei Benjamin Araule ambaye amesema kuwa idadi ya wabunge ambao wanaunga mkono kubanduliwa spika Mukenyang ni kubwa zaidi kuliko wabunge wanaopinga hoja hiyo licha ya misimamo ya vyama vya jubilee na KANU kuhusu hoja hiyo.
Araule amesema kuwa wabunge katika bunge hilo wanaoshinikiza kumwondoa Mukenya afisini wamedinda kumsikia spika huyo licha ya juhudi zake kusuluhisha tofauti hizo kupitia mazungumzo ikizingatiwa ameasalia na muda mchache kabla ya kujiuzulu ili kuanza harakati za kugombea kiti cha mwakilishi kina mama kaunti hii.