MJADALA UNAOHUSU KUBUNIWA KAUNTI MPYA YA MLIMA ELGON WAZIDI KUTOKOTA.

Mjadala wa kuongeza idadi ya kaunti kutoka arobaini na saba hadi hamsini na mbili unaendelea kuibua hisia kinzani huku wanasiasa na Wakaazi wa maeneo yanayolengwa wakiwasuta wanaopinga pendekezo hilo 

Mmoja wa wanasiasa katika kaunti ya Trans nzoia paul moiben alisema Wakazi wa eneo la mlima elgon wanahisi kutengwa katika uongozi, ugavi wa rasilimali, ajira na hata katika huduma muhimu za serkali licha kutozwa kodi kama wenzao. 

Moiben alisema kwamba pendekezo hilo si geni kwani mwaka 2019 wakenya wawili waliwasilisha ombi katika bunge la seneti kushinikiza kuongeza kwa kaunti na kwamba huu ndio wakati mwafaka wa kutekeleza 

Awali mbunge wa kimilili Didmus Baraza aliweka wazi kwamba ataunga mkono kubuniwa kwa kaunti nyingine kwenye eneo la mlima elgon kando na ile kaunti ya bungoma. 

Ikumbukwe mbunge wa Kuria mashariki Marwa Maisori aliwasilisha mswada wa kuifanyia marekebisho sura ya 98 ya katiba ili kuongeza kaunti mpya tano zikiwamo mwingi ambayo itatoka katika kaunti ya Kitui, mlima Elgon kutoka kaunti ya Bungoma na Trans nzoia, Teso kutoka kaunti ya Busia Pokot mashariki kutoka kaunti ya Pokot magharibi na kuria kutoka kaunti ya Migori