MIZOZO YAZIDI KUKUMBA CHAMA CHA FORD KENYA.
Mzozo wa uongozi katika chama cha ford kenya unazidi kutokota baadhi ya viongozi wa chama hicho kaunti ya Trans nzoia wakishinikiza mkutano wa kitaifa wa wanachama hicho kufanyika tarehe sita mwezi ujao kumchagua kiongozi wa chama hicho.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa ford kenya Peter puka kutoka eneo bunge la kwanza na mwenzake wa Saboti Anthony sikulu wanasema ni wakati wa chama cha ford kenya kuandaa kongamano la chama ambalo litawaleta pamoja wale walioasi chama hicho na pia kuimarisha democrasia
Vilevile viongozi wa chama hicho eneo la kwanza na sabaoti kaunti ya wamesema chama hicho kinahitaji kuimarisha ngome yake ya magharibi mwa Kenya na hasa Trans nzoia kama njia moja ya kukiweka tayari na katika nafasi nzuri ya uongozi mwaka ujao wakihimiza wakaazi wajitokeze kwa wingi wajisajili kuwa wapiga kura.