MIUNDO MSINGI DUNI YATATIZA 100% YA WANAFUNZI KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA.


Huenda sera ya serikali kuhakikisha asilimia 100 ya wanafunzi wanaofanya mtihani wa kitaifa kwa darasa la nane KCPE wanajiunga na kidato cha kwanza ikakosa kuafikiwa kikamilifu.
Haya ni kwa mujibu wa naibu mwalimu mkuu wa shule ya upili ya mseto ya Siyoi katika kaunti hii ya Pokot magharibi Waidhanji Kaira ambaye amesema kando na baadhi ya wanafunzi kufeli kujiunga na shule za upili ipo changamoto ya miundo msingi ya kukidhi idadi kubwa ya wanafunzi shuleni.
Amesema hali hii pia inakuwa changamoto katika kuhakikisha kanuni za kukabili maambukizi ya virusi vya corona miongoni mwa wanafunzi zinazingatiwa.
Wakati uo huo Kaira amesema kuwa wengi wa wanafunzi waliotengewa nafasi za kidato cha kwanza kwenye shule hiyo wanatoka maeneo ya mbali na ikizingatiwa ni shule ya kutwa, imekuwa changamoto kuwasajili wanafunzi hao, shule hiyo ikiishia kutegemea wanaotuma maombi ya kujiunga nayo kutoka maeneo ya karibu.