MITAA YA MABANDA TRANS NZOIA KUIMARISHWA.

NA BENSON ASWANI
Serikali ya kaunti ya Trans nzoia inalenga kuboresha miundo msingi kwenye mitaa mbali mbali ya mabanda katika kaunti hiyo.
Waziri wa ardhi katika kaunti hiyo Boniface Wanyonyi amesema kuwa serikali ya kaunti hiyo kwa ufadhili wa benki kuu ya dunia inashirikiana na mradi wa Kenya informal settlement Program ili kufanikisha lengo hilo.
Mitaa ya mabanda ambayo imeratibiwa kunufaika na mradi huo ni pamoja na shimo latewa, shanty, matisi, mitume na kipsongo.
Wanyonyi amesema kuwa ujenzi wa barabara ya kitale-endebes-swam wa kima cha shilingi milioni 4.5 utasuluhisha msongamano wa magari unaoshuhudiwa kwa sasa, kuboresha mandhari ya mji wa Kitale sawa na kuimarisha biashara baina ya mataifa ya Kenya na Uganda utakapokamilika..