MISURURU YA MIKUTANO YAANZISHWA NA WAZEE WA JAMII YA POKOT ILI KUMALIZA MIZOZO INAYOSHUHUDIWA KWENYE MIPAKA

Wazee kutoka jamii ya Pokot sasa wameanzisha misururu ya mikutano ya amani katika Bonde la Kerio ambalo linakabiliwa na utovu wa usalama na mauaji ya mara kwa mara

Kulingana na Wazee hao wanasema kuwa suluhu la kudumu ni kupitia tu mazungumzo  baina ya jamii zinazoishi katika eneo hilo

Wakizungumza baada ya kikao mjini kapenguria wazee hao wanaitaka serkali kuimarisha usalama huku wakiwataka viongozi wa kisiasa kuwa mstari wa mbele kuhubiri amani

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la wazee wa jamii ya Pokot John Mwok wazee hao wanapendekeza mazungumzo baina ya wadau mbalimbali katika sekta ya usalama ilikumaliza uhasama baina ya jamii zinazoishi katika eneo hilo

[wp_radio_player]