MIPANGILIO ‘MIBAYA’ YA KALENDA YA MASOMO YATAJWA KUCHANGIA VISA VYA MIOTO SHULENI.

Na Benson Aswani
Kutokuwapo kwa muda wa kutosha wa wanafunzi kupumzika baina ya mihula ni moja ya sababu ambayo imepelekea kushuhudiwa kwa visa vya kuteketezwa mabweni kwenye shule mbali mbali nchini.
Hayo ni kulingana na mhadhiri katika chuo kikuu cha moi mjini eldoret dr. Wilson kiptala ambaye amesema kuwa wanafunzi wanastahili kupewa muda wa kutosha wa kupumzika ili kutuliza akili na shinikizo zinazotokana na masomo.
Akiongea kwenye eneo la kapkwang’, eneo bunge la baringo kaskazini Dkt. kiptala amesema kuwa licha ya wizara ya elimu kutaka kurejesha kalenda ya masomo kama ilivyokuwa kabla ya ujio wa janga la virusi vya korona, wanafunzi wanastahili kupewa nafasi nzuri ya kupumzika.
Kiptala aidha anapendekeza muda wa kufungwa kwa shule kwa likizo fupi ya muhula wa kwanza kuongezwa hadi angalau wiki moja ili kuwapa wanafunzi muda mzuri wa kupumzika.
Wakati uo huo kiptala ambaye ni mwaniaji wa kiti cha ubunge eneo hilo amelalamikia kile amesema kuwa kudorora kwa viwango vya elimu eneo bunge hilo ambapo ameahidi kuhakikisha sekta hiyo inaimarika iwapo atachaguliwa kama mjumbe wa eneo hilo.