MIMBA ZA MAPEMA ZINGALI CHANGAMOTO POKOT MAGHARIBI.


Wito umetolewa kwa wadau katika kaunti hii ya pokot magharibi kuchangia katika kusuluhisha tatizo la mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi hasa wa kike ili kuwawezesha kukamilisha masomo yao.
Ni wito wake mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya meshack tumkou Carolyne Kiburio ambaye amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakiachia njiani masomo kutokana na mimba za mapema.
Aidha Kiburio amelalamikia uchache wa madarasa katika shule hiyo, ukosefu wa chumba cha mankuli na maktaba akitoa wito kwa wadau kuingilia kati kuhakikisha shule hiyo inashughulikiwa ili kutoa mazingira bora ya elimu kwa wanafunzi.
Wakati uo huo amesema shule hiyo sasa inatoa nafasi kwa wanafunzi wa kutwa kando na wale wanaoishi shuleni ili kuwashughulikia pia wanafunzi kutoka jamii ambazo hazimudu karo ya shule ya bweni.