MIMBA ZA MAPEMA ZIMESALIA CHANGAMOTO POKOT MAGHARIBI.


Swala la mimba za mapemamiongoni mwa wanafunzi limesalia changamoto katika kaunti hii ya Pokot magharibi.
Haya ni kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya St Bakhita Grace Akure Kakuko ambaye amesema katika shule hiyo pekee jumla ya wanafunzi 14 walifanya mtihani wa kitaifa kwa kidato cha nne KCSE wakiwa wajawazito huku wengine wakiwa wamejifungua.
Akure amelaumu pakubwa utepetevu miongoni mwa wazazi kwa ongezeko la hali hiyo ikizingatiwa nyingi ya mimba hizo zilipatikana wakati wanafunzi wakiwa likizo baada ya shule kufungwa kufuatia ujio wa janga la corona.
Amewataka wazazi kuwa makini na wanao na kutowapa uhuru mwingi bali kuwahusisha katika shughuli mbali mbali wakati wakiwa nyumbani.