MIMBA ZA MAPEMA ZATAJWA KUSALIA CHANGAMOTO POKOT MAGHARIBI.


Wadau katika sekta ya elimu wameendelea kulalamikia mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi wa kike katika shule mbali mbali kaunti hii ya Pokot magharibi hali ambayo imewapelekea wanafunzi wengi kukosa kuafikia ndoto zao maishani.
Wa hivi punde kulalamikia swala hili ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya mseto ya Sebit Samwel Kapelku ambaye amesema kuwa wanafunzi wengi werevu ambao walitarajiwa kuendeleza masomo yao wameathirika na swala hili akisema mikakati inafaa kuwekwa ili kuhakikisha linakabiliwa.
Aidha Kapelku amelalamikia swala la matumizi ya dawa za kulevya ambalo amesema lilikuwa limekithiri miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wakisambaziwa kutoka kituo cha kibiashara cha sebit hali iliyopelekea ongezeko la utovu wa nidhamu.
Hata hivyo amesema ushirikiano baina ya wadau mbali mbali ikiwemo wazazi, usimamizi wa soko hilo pamoja na idara za usalama umepelekea kupigwa hatua kubwa katika kuvikabili visa hivyo.