MIMBA ZA MAPEMA ZASALIA CHANGAMOTO KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI.


Mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi zimesalia changamoto katika shule za kaunti hii ya Pokot magharibi.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya St Anthony of Pador Sina Simon Kacheleo, swala hili limesalia changamoto katika shule hiyo hasa ikizingatiwa ni shule ya mseto, hali ambayo imewalazimu kuweka mikakati ya kukabili visa hivyo ikiwemo kuhakikisha wahusika wote wanawajibishwa.
Wakati uo huo Kacheleo amewapongeza wadau wote kwa kuhakikisha shule hiyo inaendelea kukua wakiwemo wazazi, viongozi wa kisiasa pamoja na wale wa kidini ambao amesema wamechangia pakubwa katika kuhakikisha nidhamu miongoni mwa wanafunzi.