MIKUTANO YA AMANI YAENDELEZWA KAUNTI YA BARINGO LICHA YA UGUMU WA KUWAPATA WAKAZI


Viongozi kutoka kanda ya kaskazini mwa bonde la ufa wanaendeleza misururu ya mikutano katika kaunti ya Baringo katika juhudi za kuhakikisha usalama unaimarishwa kwenye kaunti hiyo.
Hii ni baada ya serikali kusitisha oparesheni ambayo imekuwa ikiendelezwa eneo hilo ili kutoa nafasi kwa viongozi wa kanda hii kutafuta mwafaka kupitia mazungumzo na wenyeji kaunti hiyo na wakazi wa kanda hii kwa jumla.
Kulingana na spika wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Catherine Mukenyang kufikia sasa wameandaa mikutano mitatu lengo kuu likiwa kuwahimiza wakazi wanaomiliki silaha haramu kuzisalimisha.
Aidha Mukenyang amesema wanakabiliwa na changamoto ya kuwapata wakazi wa kuandaa kikao nao kutokana na hali kuwa wengi wamehama makazi yao huku wengine wakienda kuwatafutia mifugo lishe kutokana na ukame unaoshuhudiwa maeneo hayo.