MIKAKATI YAWEKWA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII TRANS NZOIA.


Waziri wa Michezo,vijana, utalii na Utamaduni Kaunti ya Trans Nzoia Aggery Chemonges amekariri kuwa wizara yake itashirikisha washikadau wote kutoka maeneo yenye vivutio vya kitalii kama njia moja ya kukuza sekta hiyo.
Akihutubu kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya Utalii ulimwenguni iliyoandaliwa eneo la Kiptogot eneo bunge la Endebess, Chemonges amesema kushirikisha jamii katika kukuza utalii kutaimarisha sekta hiyo nchini.
Aidha amesema wizara yake inashirikiana na wadau wengine katika sekta ya utalii katika kuhifadhi na kurekebisha baadhi ya nyumba zilizo kuwa za kikoloni ili kuwa moja wapo ya vivutio vya utalii mbali na kupiga jeki mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Mlima Elgon na Saiwa Swam kwenye Kaunti hiyo.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na Cate Kerubo afisa wa maswala ya utalii katika wizara hiyo akisema ipo haja ya akina Mama na vijana kukumbatia sekta ya utalii kama njia moja ya kujitafutia mapato.