MIKAKATI YA UJENZI WA BARABARA KUU YA KITALE –LOKICHAR YAENDELEZWA


Kampuni ya kutoa ushauri kuhusu ujenzi wa barabara kuu ya Kitale-morpus –Lokichar ya CGP Consulting Engineers inaendeleza vikao na wadau mbali mbali kupata maoni kuhusu mradi huo kabla ya kutekelezwa rasmi na mamlaka ya barabara kuu nchini Kenha.
Akizungumza baada ya kikao na wadau mbali mbali kaunti hii ya Pokot magharibi, afisa katika kampuni hiyo mhandisi Maina Githinji amesema kwamba baada ya kutamatika vikao hivyo watatoa ushauri kwa mamlaka hiyo kwa kutegemea maoni ambayo yametolewa na wakazi wa maeneo husika.
Githinji amesema kwamba maoni ya wananchi ambayo pia yanajumuisha mashirika mbali mbali yakiwemo yasiyo ya serikali ni muhimu katika utekelezwaji wa mradi huo kwani yatatoa picha kamili ya kile kinachohitajika kabla ya kutekelezwa rasmi.
“Tunakutana na watu wengi ambao wanahusishwa na huu mradi wa Kenha ambapo benki ya African Development Bank wameonyesha nia ya kuufadhili. Tutakuwa na vikao na wenyeji wa hapa tupate maoni ili tujue ni nini kinahitajika kabla ya kuanza kutekelezwa mradi huu.” Alisema.
Githinji amesema kuwa wakazi wa kaunti hii hasa maeneo ambako mradi huo ambao unafadhiliwa na benki African Development Bank utatekelezwa watanufaika na miradi mbali mbali itakayotokana na shughuli nzima ya ujenzi wa barabara hiyo punde utakapotekelezwa.
“Miradi mingi itakuja na huu mradi kama vile eneo la Ortum kwa sababu watu wengi wanafanyia shughuli zao kando ya barabara, tutaangalia jinisi tutaimarisha soko la eneo hili ili watu wanaofanyia shughuli zao kando ya barabara wanap[ata sehemu nzuri ya kufanyia biashara zao.” Alisema.

[wp_radio_player]