MIKAKATI INAENDELEA KUWEKWA ILIKUHAKIKISHA WALIMU ZAIDI WANAJIRIWA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBITume ya huduma kwa walimu nchini TSC inaendeleza mikakati ya kuwaajiri walimu zaidi katika maeneo yanayoshuhudia uhaba wa walimu ili kuboresha viwango vya elimu maeneo hayo.
Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Jamleck Muturi ambaye pia amewataka wazazi katika kaunti hii ya Pokot magharibi kutilia maanani elimu ya wanao na kuhakikisha kuwa wanawapeleka shuleni.
Aidha Muturi amesema tume hiyo inaweka mikakati ya kuhakikisha usalama wa walimu katika kaunti hii kwa kuwatuma walimu ambao ni wenyeji kuhudumu maeneo ya mashinani, pamoja na kushirikiana na serikali ya kaunti kuhakikisha hilo linaafikiwa.
Kwa upande wake afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Nancy Macharia amesema TSC imeanzisha mpango wa kutoa mafunzo kwa wanafunzi kupitia mitandaoni ikiwa ni njia moja ya kukabili tatizo la uhaba wa walimu pamoja na vifaa vya masomo, mpango huo ukitarajiwa kufanyiwa majaribio kwa shule 12.
Aidha amesema tayari wameanza kutoa mafunzo kwa walimu kuhusu jinsi ya kufanikisha mpango huo.