MIITO YAENDELEA KUTOLEWA KWA WAKAZI POKOT MAGHARIBI KUJISAJILI KUWA WAPIGA KURA.


Viongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kutoa wito kwa wakazi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kuwa wapiga kura katika zoezi la mwezi mmoja la usajili wa wapiga kura wapya ambalo linaendelezwa na tume ya uchaguzi na mipaka IEBC.
Wa hivi punde kutoa mwito huo ni spika wa bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi ambaye pia amewataka wadau mbali mbali wakiwemo machifu na manaibu wao pamoja na viongozi wa kidini kutumia nafasi zao kuwashinikiza wananchi kujisajili kwa wingi.
Wakati uo huo Mukenyang amewataka wafugaji wa mifugo waliohamia taifa jirani la Uganda kutafutia mifugo yao lishe kutekeleza shughuli zao kwa zamu ili pia kupata nafasi ya kujisajili kabla ya kukamilika rasmi zoezi hilo.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwakilishi wadi maalum Elijah Kasheusheu ambaye amesema kuwa ni kupitia tu kujisajili kuwa wapiga kura ndipo wananchi wataweza kutekeleza haki yao ya kidemokrasia ya kuwachagua viongozi wanaotaka katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.