MIITO YA KUPATANA RAIS KENYATTA NA NAIBU WAKE YAZIDI KUTOLEWA.
Tangazo la baraza la maaskofu kwamba liko tayari kuwapatanisha rais uhuru kenyata na naibu wake Wiliam Ruto limetajwa kuwa lenye umuhimu mkubwa katika kuleta umoja amani na utangamano wa taifa.
Mshirikishi wa uongozi na amani katika jamii ya kalenjin katika kaunti ya Trans nzoia Michael seronoi amesema ni busara kwa rais kenyata na ruto kuweka tofauti zao kando na kuhudumia wakenya jinsi alivyofanya tu katika mahakama ya kimataifa ya icc walipokuwa na kesi wakati huo pamoja.
Hata hivyo mshirikishi huyo wa uongozi anasema kuwa iwapo hawatachukua hatua za haraka huenda wakarejea tena icc
Ikumbukwe siku chache zilizopita naibu wa rais wiliam ruto alisema yuko tayari kuridhiana na rais uhuru kenyata bila masharti yoyote
Awali rais uhuru kenyata alimtaka ruto ajiuzulu ikiwa haridhishwi na utendakazi wa serkali anayoihudumia hata hivyo ruto alisema kwamba hatajiuzulu hatua iliyoweka wazi kwamba uhusiano wao bado una madoa.