MIITO YA AMANI YATOLEWA IEBC IKIENDELEA KUWATANGAZA WASHINDI WA UCHAGUZI.
Miito imeendela kutolewa kwa wananchi kuendela kuwa na subira wakati tume ya uchaguzi IEBC inapoendelea kusubiriwa kutangaza matokeo ya wawaniaji wa viti mbali mbali katika shughuli ya upigaji kura ambayo iliandaliwa jumanne juma hili.
Ni wito ambao umetolewa na mbunge mteule katika kaunti ya Trans nzoia Milka Sugut ambaye aidha ameitaka tume ya IEBC kuzingatia malalamishi ambayo yanatolewa na wananchi kuhusiana na maswala mbali mbali ambayo yanaibuliwa kuhusiana na shughuli nzima ya uhesabu wa kura.
Wakati uo huo amewapongeza wakazi wa eneo hilo kwa kujitokeza kwa wingi kuhakikisha kwamba chama cha UDA kinazoa viti vingi vilivyowaniwa eneo hilo huku akielezea matumaini ya kinara wa chama hicho William Ruto kutwaa wadhifa wa urais.
Wito kama huo pia ulitolewa na waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa.