MIITO YA AMANI YAENDELEA KUTOLEWA SIKU CHACHE KABLA YA UCHAGUZI MKUU.
Vijana katika Kaunti ya Pokot Magharibi wameapa kutokubali kushirikiana na wanasiasa wanaowatumia kuvuruga mikutano ya wapinzani wao kwa manufaa yao ya binafsi.
Wakiongozwa na Stephen machar wakaazi wa kaunti hii wameendelea kuwashutumu wawaniaji wanaowatumia vijana kuzua rabsha katika mikutano ya wapinzani wao akiwataka wakaazi pamoja na wawaniaji kudumisha Amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Wakati huo huo wakaazi hao wametoa ombi kwa wenzao kutoka taifa jirani la Uganda kukoma kuwatuma watoto wadogo kuchunga mifugo.
Vile vile wametoa wito kwa wakaazi kutoegemea Zaidi siasa na kusahau mifugo wao kuibiwa kwani hali hii inapelekea hasara katika jamii taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu wa agosti 9.
Wakati uo huo wamewataka wakaazi mpakani pa Uganda na kaunti hii kushirikiana na machifu kuona kwamba masomo yanapewa kipau mbele na kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wote watakaopatikana wakiwatuma watoto wadogo kuchunga ng’ombe badala ya kwenda shuleni.