MIITO YA AMANI YAENDELEA KUTOLEWA CHINI YA MASAA 24 KABLA YA UCHAGUZI WA JUMANNE.


Ikiwa yamesalia chini ya masaa machache tu kabla ya uchaguzi mkuu wa hapo kesho jumanne, viongozi kaunti hii ya Pokot magharibi wameendelea kutoa wito kwa wananchi kudumisha amani ili kuwe na mazingira bora ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi huo.
Wakliongozwa na naibu gavana kaunti hii Nicholas Atudonyang, viongozi hao wamesema kuwa wananchi wanapasa kuelewa demokrasia ya kuwa si kila mwaniaji atachaguliwa katika uchaguzi huo na wanapasa kukumbatia uamuzi wowote utakaofanya.
“Nawahimiza wananchi ya kwamba tufanye uchaguzi wa amani. Tunajua wakati huu ni wakati kila mtu anavuta upande wake lakini tunawaomba wakazi waelewe process ya demokrasia ya kujua ya kwamba tutakuwa na washindi na wale ambao watashindwa.” Amesema Atudonyang.
Aidha Atudonyana amewapongeza wanasiasa waliojitokeza kuwania viti vya uongozi katika kaunti hii ya Pokot magharibi kwa kuendesha kampeni za amani kipindi chote cha kampeni ambacho kilikamilika jumamosi wiki iliyopita.
Kauli kama hiyo pia ilitolewa awali na seneta wa kaunti hii Samwel poghisio aliyehudhuria ibaada ya maombi katika kanisa la redeemed gospel church mjini makutano kapenguria kaunti ya pokot magharibi na ambaye amewatahadharisha wananchi kutopatikana wakisoma vijikaratasi vya chuki vinavyodaiwa kusambazwa hasa eneo la bonde la ufa.
“Nimesiki hapa rift valley kuna watu wanasambaza makaratasi ya kuchochea. Tafadhali wananchi mkiona makaratasi kama hayo usipatikane ukiyasoma, tuachane nayo. Makaratasi kama hayo ni ya kuharibu amani Kenya.” Amesema Poghisio.
Poghisio ameongeza kuwa, “Tunataka kuwaomba watu kwamba tafadhali kama kuna watu ambao wameanzisha mambo kama hayo wasiwe wanatuletea shida ya kuchochea watu katika wakati wa uchaguzi.”