MIGAWANYIKO YAENDELEA KATIKA BARAZA LA WAZEE WA KEIYO KUHUSU KUIDHINISHWA JOSEPH BOINET KUWANIA UGAVANA ELGEYO MARAKWET.


Siku chache baada ya wazee wa jamii ya keiyo kumwidhinisha aliyekuwa inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinet kuwania kiti cha ugavana katika kaunti ya Elgeyo marakwet, baadhi ya wazee na wakazi wa kaunti hiyo wameendelea kupuuzilia mbali hatua hiyo.
Wakiongozwa na William Kiptarus baadhi ya wakazi wa eneo la Keiyo kaskazini na Keiyo kusini wamedai kuwa hawakuhusishwa katika mazungumzo ya kujadili mustakabali wa siasa wa jamii hiyo.
Aidha baadhi ya wazee wamedai kuwa waliomwidhinisha Boinet hawana uwezo wa kutoa uamuzi kwa niaba ya jamii nzima.
Hata hivyo baadhi ya vijana kutoka jamii hiyo wamesema hatua ya wazee hao ilifaa wakielezea imani kuwa Boinet atakuwa kiongozi bora wa kaunti ya Elgeyo Marakwet.