MIGAWANYIKO YAANZA KUSHUHUDIWA KATIKA MUUNGANO WA KENYA KWANZA.


Baadhi ya wanachama wa muungano wa kenya kwanza Trans nzoia wamesuta matamshi ya mwenyekiti wa UDA Johnstone Muthama aliotoa juzi wakidai huenda ikaleta mshike mshike chamani humo.
Wakiongozwa na luke naibei pamoja na imaculate shamala wanachama hao wanadai kuwa matamshi ya muthama kuashiria hamna makubaliano yoyote na vyama vya Ford kenya na ANC huenda ikapelekea wafuasi wa vyama hivyo kugura muungano huo.
Wanamtaka naibu raisi william ruto kujitokeza na kuelezea makubaliano yao ili kupunguza tumbo joto linaloshudiwa kwa sasa.