MIFUGO WALIOIBWA KERIO VALLEY WAREJESHWA.
Na Benson Aswani
Mifugo tisa kati ya hamsini walioibwa wamerejeshewa wenyewe katika eneo la kerio valley kaunti ya Elgeyo marakwet
Hayo ni kwa mjibu wa naibu kamishna wa Marakwet mashariki Simon Osumba ambaye amesema kuwa maafisa wa polisi wakishirikiana na wakaazi kutoka kaunti ya Baringo na Elgeyo marakwet pamoja na wazee wa amani walirejesha mifugo baada ya kuibwa mnamo siku ya ijumaa na wavamizi wanaoaminika kutoka kaunti ya Baringo
Osumba aidha ameongeza kuwa kuna matumaini ya kurejesha mifugo hao iwapo ushirikiano kama huo utaendelea siku ya leo.