MGOMO WA WAHUDUMU WA AFYA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI YAINGIA SIKU YA NNE

POKOT MAGHARIBI


Mgomo wa wahudumu wa afya katika kaunty ya Pokot Magharibi sasa umeingia siku yake ya nne huku wahudumu hao wakitarajiwa kuwahutubia wanahabari.
Madaktari hao wanalalamikia kutolipwa marupurupu, bima ya afya inayoshughulikia magonjwa sugu kama vile corona miongoni mwa malalamiko mengine.
Kulingana na katibu mkuu wa chama hicho tawi la kaskazini mwa bonde la ufa Dkt Ismael Aiyabei ni kwamba wameafikia hilo baada matakwa yao matatu kukosa kuafikiwa na serikali ya kaunti hii.
Kwenye mahojiano ya kipekee ndani ya kipindi tawala cha mpigo wa kalya radio wiki jana Aiyabei alisema kuwa matakwa hayo waliafikiana baina yao na serikali ya kaunti hiyo tarehe 6 mwezi julai mwaka wa 2017.
Awali Seneta wa kaunti hii ya Pokot Magharibi Samwel Poghisio awali aliendeleza shutuma zake dhidi ya uongozi wa kaunti hii kwa madai ya kutelekeza hospitali ya Kapenguria na madaktari kwa jumla katika mikakati ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Akizungumza na kituo hiki Poghisio amesema kuwa serikali ya Gavana John Lonyangapuo imekosa kufanikisha juhudi za kuiweka hospitali hiyo katika hadhi inayostahili licha ya kuwepo fedha za kutosha.
Poghisio amesema kuwa huenda hospitali hiyo ikarejeshwa chini ya usimamizi wa serikali kuu iwapo uongozi wa gavana Lonyangapuo hautawajibika katika usimamizi wake.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ambaye amesema madaktari katika hospitali hiyo hawana vifaa vya kujikinga dhidi maambukizi ya corona hali ambayo inawapelekea kuhofia kuwashughulikia washukiwa wa visa hivyo.
Ikumbukwe takriban wahudumu wa afya 32 wamefariki kutokana na ugonjwa wa covid 19.