MGOMO WA MADAKTARI WAINGIA SIKU YAKE YA SITA

POKOT MAGHARIBI


Mgomo wa madaktari katika kaunti ya Pokot Magharibi ambao uling’oa nanga siku ya ijumaa wiki iliyopita umeingia siku ya sita.
Waziri wa afya kaunty ya Pokot Magharibi Jackson Yaralima amesema kwamba matakwa ya madaktari hao yanashughulikiwa na iwapo mgao wao hautapatikana basi itawalazimu tena kurejelea kwenye vikao na kujadiliana.
Awali katibu wa muungano wa madaktari KMPDU kaskazini mwa bonde la ufa Ishmael Ayabei, alitaja mgomo huo kuchochewa na hali ngumu ya kufanyia kazi wakati huu wa janga la corona sawa na kutotekelezwa kwa mkataba wa maelewano baina yao na serikali ya kaunti uliotiwa sahihi mwaka 2017.
Kuhusu mgao uliotolewa na serkali kuu ili kukabiliana na janga la corona kwenye kila kaunti waziri Yaralima amedhibitisha kwamba kaunti ya Pokot Magharibi ilipokea milioni sabini na tano nukta mbili tisa na kwamba kiwango kidogo cha pesa kilitumika katika kununua vitanda pamoja na vifaa vingine vya afya.