MGOMBEA KITI CHA UBUNGE KAPENGURIA LUCY LOTEE AAGA DUNIA.
Jamii ya aliyekuwa mwakilishi wadi maalum Lucy Lotee inaendelea kuomboleza kifo chake baada yake kuaga dunia hiyo jana katika hospitali ya Kapenguria kaunti hii ya Pokot magharibi.
Kulingana na mwanawe Allan Lotee, mwenda zake alizidiwa akiwa amelazwa katika hospitali hiyo kutokana na tatizo lake la muda mrefu la figo ambapo alikuwa amewekewa kifaa cha kumsaidia kupumua.
Viongozi wa kisiasa kaunti hii wakiongozwa na mgombea kiti cha mwakilishi wadi ya Kapenguria Jane Ruto wameendelea kumwomboleza mwenda zake wakilaumu uhaba wa vifaa vya matibabu katika hospitali ya Kapenguria kuwa chanzo cha kifo chake.
Ikumbukwe katika siku zake za uhai marehemu amekuwa msitari wa mbele kupigania uboreshwaji wa huduma katika hospitali ya Kapenguria hasa kitengo cha kuwashughulikia wagonjwa wa figo pamoja na uhaba wa mitambo ya oksijeni.