MGOMBEA KITI CHA UBUNGE ENDEBES KAUNTI YA TRANSNZOIA AHAIDI KUWATAFTA WAWEKEZAJI IWAPO ATACHAGULIWA



Kiongozi na musomi kutoka eneo bunge la Endebess Kaunti ya Trans Nzoia Pius Gumo amesema yuko tayari kuwatafuta waekezaji iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge ili kupiga jeki eneo bunge hilo ikiwemo suala la ajira kupitia viwanda.
Akiongea alipokutana na makundi ya kina Mama kutoka eneo bunge hilo,Pius Gumo amesema Endebess imesalia nyuma kutokana na uongozi duni wa Mbunge alioko kwa sasa huku akiongeza kwamba wakati umewaida wa kuleta mabadiliko, akiwarai wananchi kumuunga mwaniaji wa Urais kupitia muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga ifikapo Agosti tisa.
Ni hoja iliyotiliwa mukazo na aliyekuwa Mbunge wa Westlands mjini Nairobi Fred Gumo ambaye amewataka Wakenya kumpigia kura Raila Odinga na Martha Karua kwa kile anasema hao ndio wataweza kupambana na ufisadi na vile vile kufufua uchumi.