MGOGORO WATISHIA KUATHIRI UTHABITI WA CHAMA CHA FORD KENYA


Pana haja ya uongozi wa chama Ford kenya kuondoa kesi mahakamani dhidi ya mrengo wa mbunge wa tongaren Dkt Eseli Simiyu na kuruhusu uchaguzi wa mashinani kufanyika kabla ya mkutano wa baraza kuu la wajumbe wa chama hicho.
Haya ni kwa mujibu wa viongozi wa chama cha Ford kenya ambao wanaegemea mrengo huo.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho kwenye eneobunge la Kwanza kaunti ya Trans nzoia Peter Puka viongozi hao wamesema kuwa mzozo umelemaza shughuli za chama na hata kuibua uhasama miongoni mwa wanachama.
Matamshi ya Puka yameungwa mkono na mshirikishi wa chama hicho kwenye eneobunge la Kiminini Wekesa Lusatia.