MFUMO WA BOTTOM UP WAPIGIWA UPATU BARINGO.

Na Benson Aswani
Viongozi katika kaunti ya Baringo wanazidi kupigia debe mfumo wa kuimarisha uchumi unaopendekezwa na naibu rais Dkt William Ruto wa bottom up ecomonic model.
Kulingana mwaniaji wa ubunge kwenye eneo bunge la Eldama ravine Musa Sirma mfumo huo utawapiga jeki wafanyabiashara wadogo wadogo na pia utatoa nafasi za kazi kwa vijana.
Sirma aidha ameahidi kuweka kipau mbele mpango wa uimarishaji wa miundo msingi kwenye eneo bunge hilo iwapo ataibuka mshindi kwenye uchaguzii mkuu wa mwaka ujao.