MCHUNGAJI AKAMATWA BAADA YA KUMPACHIKA MIMBA MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA MOI’S BRIDGE


Mchungaji wa kanisa moja katika mtaa wa Reli viungani mwa mji wa Moi’s Bridge Christopher Juma mwenye umri wa miaka 45 amekamatwa na polisi wa kituo kidogo cha Mashine baada ya kumpachika mimba mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 16.
Inadaiwa mwanafunzi huyo aligunduliwa kuwa na uja uzito na mwalimu wake alipoenda shuleni.
Kulingana na mwanafunzi huyo ni kwamba mchungaji huyo alimhadaa na baadaye kushiriki tendo la ndoa naye.
Ni kisa ambacho kimedhibitishwa na naibu chifu wa kata hiyo Carolyn Vugusta ambaye amekashifu vikali kitendo hicho.
Kisa hiki kimewaacha wakaazi vinywa wazi huku wakiita serikali kuchukua hatua kali za kisheria dhiti ya mshukiwa.