MCHANGANUZI WA KISIASA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI AELEZEA MANUFAA YA BBI KWA TAIFA


Idadi ya mabunge ya kaunti hitajika katika kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba ikiwa tayari imeafikiwa, wadau mbali mbali wameendelea kukosoa mbinu iliyotumiwa kuhakikisha waakilishi wadi wanapitisha mswada huo.
Akizungumza na kituo hiki, wakili philip magal amesema kuwa hatua hii imeafikiwa baada ya rais uhuru kenyatta na kinara wa chama cha odm raila odinga kuwaahidi viongozi hao ruzuku ya magari, akipongeza tume ya kuratibu mishahara ya umma src kwa kutaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria.
Hata hivyo magal ameelezea manufaa ya mchakato wa bbi kwa taifa ikiwemo kutoa suluhu kwa swala la ukabila analosema limekithiri nchini, pamoja na kuleta raslimali zaidi maeneo ya mashinani.
Wakati uo huo amewataka wananchi kutoegemea mirengo ya siasa katika kutoa maamuzi wakati wa kura ya maamuzi kuhusu marekebisho ya katiba, na badala yake kupiga kura kulingana na jinsi wanavyoelewa ripoti ya bbi.