MCHAKATO WA KUFANYIA KATIBA MAREKEBISHO ANDALIWA BAADA YA UCHAGUZI MKUU UJAO WA 2022 ASEMA DKT KIBUNGUCHI


Mbunge wa Likuyani katika kaunti ya Kakamega Dkt Enock Kibunguchi amependekeza mchakato wa kufanyia katiba marekebisho kuandaliwa baada ya uchaguzi mkuu ujao wa 2022.
Akizungumza na wanahabari, Kibunguchi amependekeza kwa wananchi kuendelea kupewa nafasi ili kuendelea kuwasilisha maoni na mapendekezo yao kuhusu baadhi ya vipengele kwenye mswada huo kabla ya kufanyika kwa kura ya maamuzi iwapo itaandaliwa.
Kibunguchi kadhalika ametoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuzingatia uamuzi wa mahakama kuu uliofutilia mbali BBI kabla ya kuikashifu idara ya mahakama.