MBUNGE WA SOY CALEB COSITANY AMEAPA KUPINGA MSWADA WA KUREJESHA USHURU MWAKA UJAO

UASIN GISHU


Mbunge wa Soi Caleb Kositany ameapa kupinga mswada wa kurejesha ushuru wa zamani iwapo mswada huo utawasilishwa katika Bunge la kitaifa kwenye kikao maalum kinachotarajiwa kuandaliwa wiki ujao.
Akizungumza na wanahabari Kositany amesema wakenya wanateseka kutokana na athari za janga la Korona na haitakuwa bora kuwaongezea ushuru wakati wanapitia hali ngumu ya maisha.
Kositani aidha amependekeza kuwa ushuru huo ubakie jinzi ulivyo kwa sasa hadi pale biasha na hali ya uchumi itakapoimarika.
Kositany aidha amesema kuwa itakuwa bora fedha zinazotumika kuidhinisha ripoti ya BBI zitumike kushughulikia janga la korona.