MBUNGE WA SIRISIA NA MWAKILISHI WADI YA LWANDANYI WATAKIWA KUSULUHISHA TOFAUTI ZAO.


Mbunge wa Siria katika kaunti ya Bungoma John Waluke na mwakilishi wadi ya Lwandanyi Tony Baraza wametakiwa kuzika tofauti zao za kisiasa na kutekeleza maendeleo.
Wakizungumza mjini Lwandanyi wakiongozwa na Mourice Manyasi wakazi wa eneo hilo wameeleza kutoridhishwa na tofauti baina ya wawili hao na kuwahimiza kuangazia zaidi miradi ya maendeleo.
Aidha wakazi hao wamesema kuwa ipo haja kwa wawili hao kufanya mazungumzo na kusuluhisha tofauti hizo kwa manufaa ya wenyeji waliowapigia kura.