MBUNGE WA SABAOTI ASUTWA KWA KULIPAKA TOPE JINA LA SENETA WA TRANSNZOIA


Seneta wa kaunti ya Trans nzoia Michael Mbito amemsuta mbunge wa Saboti Caleb Amisi kwa madai ya kulipaka tope jina lake badala ya kutangaza sera kwa wapiga kura.
Mbito ambaye pia ametangaza nia ya kuwania ubunge wa saboti katika uchaguzi mkuu wa mwezi agosti amesema Amisi ni mwanachama wa kamati ya usalama bungeni na kuwa anatumia wadhifa huo kujipigia debe kisiasa.
Aidha Mbito amesema kuwa Amisi anafahamu kwamba hatoweza kuhifadhi kiti hicho na sasa anatumia mbinu za kuwachafulia jina wapinzani wake akikariri kwamba yuko tayari kumenyana kisiasa naye katika uchaguzi mkuu wa agosti 9.